-->

Type something and hit enter

On
 OFISA Habari wa Klabu ya KMC Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Oktoba 30 dhidi ya Gwambina FC.


KMC inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wao ulioppita uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ikiwa ipo nafasi ya 8 na pointi 11 inakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 na pointi 9 zote zimecheza mechi nane.
 
Christina amesema:-"Licha ya kupoteza mchezo wa ligi dhidi Yanga, wachezaji wako tayari kuivaa Gwambina ili kupata pointi tatu muhimu.

"Maandalizi ya mwisho yamekamilika na wachezaji wote wana  morali nzuri kuelekea katika mchezo huo na lengo ni kuhakikisha kuwa ushindi unapatikana ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu msimu wa 2020/2021.

"Kuhusu afya za wachezaji, ziko vizuri na hakuna mchezaji yeyote mwenye majeruhi na kikosi kizima kiko kamili kwa ajili ya mchezo huo hivyo ni jukumu la mwalimu kuona nani ataweza kuwakilisha kwenye mchezo huo."

Click to comment
 
Blog Meets Brand