Kipchoge Ashindwa Kutetea Taji London Marathon-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kipchoge Ashindwa Kutetea Taji London Marathon-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

Eliud Kipchoge bingwa wa mbio za marathon ameshindwa kutetea taji lake la London marathon Jumapili baada ya kuishiwa nguvu katika kilomita 35 za mbio hizo na kujikuta akimaliza katika nafasi ya nane.

 

Shura Kitata wa Ethiopia alitwaa ushindi kwa kumponyoka Mkenya Vincent Kipchumba katika sekunde za mwisho kabisa na kumaliza mbio hizo katika muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 41. Kepchumba alimaliza wa pili sekunde moja baadaye na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mkimbiaji mwingine kutoka Ethiopia, Sisay Lemma, katika muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 45.

 

Akizungumza baada ya mashindano hayo, Kipchoge alisema, “Nimesikitika sana. Nilikuwa na tatizo na sikio langu la kulia baada ya kuziba na kisha nikawa na maumivu ya tumbo na matatizo ya nyonga… Kulikuwa na baridi lakini silaumu mazingira hayo…”

 

Mbio za London marathon zilielekea kuwa kali mwaka huu zikiwapambisha Eliud Kipchoge na Kenenisa Bekele wa Ethiopia ambao walidhaniwa kuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda katika mbio hizo. Lakini hali ilianza kubadilika siku mbili kabla ya mbio pale Bekele alipotangaza kujitoa katika mbio hizo kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.

 

Kujitoa kwa Bekele kuliuacha uwanja wazi kwa Kipchoge na ilielekea hivyo kwa sehemu kubwa ya mbio hizo ambazo mwaka huu hazikutumia njia ya kawaida badala yake ilikuwa mizunguko ya eneo maalum lililotengwa.

 

Lakini hali ilianza kubadilika katika kilomita ya 35 pale Kipchoge alipoanza kupunguza kasi na kundi la akina Kitata, Kepchumba, Lemma na wengine wakachukua fursa hiyo kumtoka haraka bingwa huyo wa dunia.

The post Kipchoge Ashindwa Kutetea Taji London Marathon appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz