-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

AKITARAJIWA kutua leo Alhamisi saa 4 usiku, kocha mkuu mpya wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amewatumia ujumbe mkubwa mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kwa pamoja watafanya makubwa.

Kauli hiyo aliitoa kocha huyo akiwa njiani kutua hapa nchini akitokea Canada ambapo makazi yake yalikuwa huko.

Kocha huyo anakuja kuifundisha timu hiyo baada ya kufikia makubaliano mazuri na mabosi wa Yanga akichukua nafasi ya Mserbia, Zlatko Krmpotic aliyetimuliwa hivi karibuni.

“Ninajivunia kuwa kocha mpya wa Yanga, timu yenye historia nzuri ambayo mashabiki wake ni wazuri.“Yanga ni kati ya timu bora katika Ukanda wa Afrika, kwa pamoja tutafanya makubwa,” alisema Kaze.

 

Kaze atatua leo na moja kwa moja atajiunga na kambi ya Yanga iliyowekwa kwenye Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam tayari kwa ajili ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho.

WILBERT MOLANDI, Dar |SPOTI XTRA

The post Kaze Aahidi Makubwa Yanga appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand