-->

Type something and hit enter

On
Mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) mwaka 2015 KayumbaJuma, amesema ilibaki kidogo mwigizaji nyota Irene Uwoya awe meneja wake, lakini maneno ya watu yalimkimbiza.

 

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Msanii huyo alisema Uwoya alionesha nia ya kumsimamia kwenye muziki wake ila kutokana na namna walivyokuwa yakaibuka maneno kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanatoka pamoja.


“Uwoya alitaka kunisimamia katika muziki wangu kwa hiyo tukaanza kupiga picha na kuweka kwenye mitandao ndipo maneno yakaibuka kuwa tunatoka pamoja na yeye hakuyapenda kwa sababu ni mtu mwenye familia yake hivyo akaamua kuachana na mimi,” alisema Kayumba akizungumza na Wasafi Tv.


Alisema kwa sasa anapambana mwenyewe na meneja wake ingawa bado hajapata uwekezaji wa kutosha kufikisha mbali muziki wake.Click to comment
 
Blog Meets Brand