-->

Type something and hit enter

On
 MECKY Maxime,  Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa maandalizi ambayo wameyafanya yanawapa uhakika wa kusepa na pointi tatu mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. Leo Oktoba 14, Kagera Sugar inajitupa Uwanja wa Majaliwa kusaka pointi tatu muhimu ikiwa ni mzunguko wa sita baada ya ule wa tano kukamilika.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Timu zote zinakutana uwanjani zikiwa na matokeo yanayofanana kwenye mechi zao zilizopita ambapo Kagera Sugar wageni wametoka kutunguliwa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex huku wenyeji wao Namungo wakitoka kutunguliwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Majaliwa.


Maxime amesema:"Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa ila tupo tayari kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja, mashabiki watupe sapoti."


Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara,  Kagera Sugar ipo nafasi ya 13 na pointi 4 inakutana na Namungo iliyo nafasi ya 9 na pointi 6.

Click to comment
 
Blog Meets Brand