-->

Type something and hit enter

On
 LEO Oktoba 4, Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 wanakibarua cha kumenyana na JKT Tanzania mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambao utakuwa ni wa kisasi.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

JKT Tanzania ambao ni wenyeji wataingia uwanjani wakiwa na hasira za kupoteza mchezo wao uliopita kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union huku Simba wakiwa na kidonda cha kutunguliwa bao 1-0 msimu wa 2019/20 walipokutana na JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru hivyo wataingia na roho ya kisasi.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amsema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utapigwa majia ya saa 10:00 jioni.

“Tutakuwa na mchezo mgumu lakini hatuna mashaka tunaamini tutafanya vizuri mashabiki watupe sapoti katika hilo,” amesema.

 Wakiwa wamekutana mara nne tangu msimu wa 2018/19 kwenye mechi nne, Simba imeshinda mechi tatu na imepoteza mechi moja huku yakipatikana jumla ya mabao nane ambapo Simba imefunga mabao sita na JKT Tanzania imefunga mabao mawili.

Kocha wa JKT Tanzania, Abdalah Mohamed,’Bares’ amesema kuwa wanaamini watapambana kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

Matokeo yao yalikuwa namna hii:- 2018/19, JKT Tanzania 0-2 Simba, Simba 1-0 JKT Tanzania.2019/20 JKT Tanzania 1-3 Simba, Simba 0-1 JKT Tanzania

Click to comment
 
Blog Meets Brand