-->

Type something and hit enter

On
 KLABU  ya Barcelona imetangaza rasmi aliyekuwa Rais wao, Josep Maria Bartomeu, amejiuzulu nafasi hiyo pamoja na bodi yote ya wakurugenzi.

 

Bartomeu, 57, amekuwa Rais wa Barcelona tangu mwaka 2014, lakini homa  ya kuachia kiti hicho iliongezeka majira ya kiangazi mwaka huu baada nyota wa timu hiyo, Lionel Messi, na wachezaji wengine wa Barcelona kukosoa hadharani  uongozi wake hasa klabu hiyo ilivyokuwa inafanya sajili zake.

 

Uchaguzi utapangwa ndani ya siku 90 zijazo ili kuziba nafasi ya rais huyo.  Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kupoteza mechi ya ligi   nyumbani  kwenye uwanja wa Nou Camp dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Real Madrid, kwa kipigo cha magoli 3-1.


Habari zinaeleza kuwa nyota wa kikosi hicho Messi naye ni chanzo cha kiongozi huyo kubwaga manyanga kwa kuwa kwenye sekeseke la Messi kutaka kuibukia Manchester City alimtaa kuwa sababu ya timu kuboronga.


Messi alikubali kubaki ndani ya timu hiyo kwa kile alichoeleza kuwa hakutaka kwenda mahakamani kuzozana na timu yake ambayo imemlea.

Click to comment
 
Blog Meets Brand