-->

Type something and hit enter

On
 BEKI kisiki  ndani ya kikosi cha Liverpool, Virgil Van Dijk, anaweza kukaa nje miezi saba hii ikimaniisha huenda akazikosa mechi zote zilizosalia msimu huu, baada ya jana kuchezewa rafu mbaya na mlinda mlango wa Everton Jordan Pickford.


Rafu hiyo alichezwa kwenye mechi ya Ligi Kuu England , Uwanja wa Goodison Park wakati Liverpool ikilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.

Aidha Liverpool wameitaka Bodi ya Ligi England kuwapa maelezo ya kina ni kwa jinsi gani VAR imefikia makubaliano ya kukataa goli la dakika za jioni la nahodha wao Jordan Henderson ambalo inaelezwa alikuwa ameotea.

Na kwanini mwamuzi Michael Oliver na VAR hawakumuadhibu Golikipa Everton Pickford, kwa rafu mbaya aliyomchezea VVD.

Liverpool kwa sasa imeanza kwa mwendo wa kusuasua ambapo wakiwa ni mabingwa watetezi wapo nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikiwa mikononi mwa Everton.

Pia inakumbukumbu ya kuchapwa mabao 7-2 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Aston Villa jambo ambalo linampa wakati mgumu Jurgen Klopp kutetea taji lake kwa msimu wa 2020/21 licha ya kwamba ligi bado mbichi.

Click to comment
 
Blog Meets Brand