"Hii shule iliyoungua imekaguliwa juzi"- Zimamoto - EDUSPORTSTZ

Latest


 

"Hii shule iliyoungua imekaguliwa juzi"- Zimamoto

 
 

Bweni la shule ya Sekondari ya wasichana ya Uchira Islamic iliyoko wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, limeteketea kwa moto jioni ya Oktoba 16, 2020, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana mpaka sasa na hakuna kifo wala madhara kwa mwanafunzi yeyote.


Akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, hii leo Oktoba 17, 2020, Inspekta Abraham Ntezidyo, kutoka Jeshi la Zimamoto mkoa wa Kilimanjaro, amesema kuwa taarifa za moto huo walizipata jana jioni majira ya saa 12:00 na moto umeteketeza jumla ya vitanda 25 ambavyo walikuwa wakilala wanafunzi 50.


"Athari kubwa ni kwenye vitu vya wanafunzi na vitanda, wanafunzi hawakuwepo bwenini walikuwa wameenda Msikitini kwa ajili ya swala ya jioni, mpaka sasa hivi tunaendelea na uchunguzi wa moto huo ili kubaini chanzo na moto ulipoanzia", amesema Inspekta Abraham.


Aidha Inspekta Abraham ameongeza kuwa, "Hapa wanafunzi wako katika hali ya mshtuko, mikakati iliyopo tunakagua shule moja baada ya nyingine kwa kushirikiana na vyombo vingine na hata hii iliyoungua tunavyozungumza imekaguliwa juzi tu hata wiki haijaisha, lakini bahati mbaya imeungua, vyanzo vya moto viko vingi kuna umeme, hujuma, kuna vingine vinasababishwa kwa makusudi".Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz