-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

SHIRIKISHO  la Soka Barani Afrika (CAF) limelazimika kuahirisha fainali ya Ligi ya Mabingwa iliyokuwa ichezwe Novemba 6, 2020, kutokana na kucheleweshwa kwa pambano la marudio la nusu fainali baina ya Zamalek ya Misri na Raja Casablanca ya Morocco kufuatia wachezaji zaidi ya 10 wa Raja kupatikana na Covid-19.

Nusu fainali hiyo ilikuwa imepangwa kuchezwa  leo Oktoba 31 lakini kwa sasa itasubiri hadi wachezaji wa Raja wapone.

 Fainali hiyo imesogezwa mbele ili kutoa fursa kwa mechi za kufuzu AFCON zitakozochezwa mwezi ujao.

Timu ya Al-Ahly imetangulia kwenye fainali ikisubiri mshindi kati ya Zamelek au Raja Casablanca ambapo katika matokeo ya mechi ya kwanza Zamalek anaongoza kwa bao 1-0.

The post Fainali Ligi ya Mabingwa Yapigwa Kalenda appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand