-->

Type something and hit enter

On
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas mchana wa Jana tarehe 15 Oktoba, 2020 amefika katika studio za producer S2KIZZY ambazo usiku wa kuamkia jana kulitokea uvamizi ambapo watu kadhaa waliumizwa na uharibifu wa vifaa vya studio.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Baada ya kujionea hali halisi Dkt. Abbas amesisitiza watu kuiheshimu sanaa na kwamba sanaa ni kazi kama ilivyo kazi zingine  huku akiahidi kuwa polisi wanakamilisha uchunguzi ili haki itendeke.  “Tukio hilo liko polisi, nimeagiza uchunguzi ufanyike haraka na hatua kali zichukuliwe dhidi ya waliohusika na tukio hilo.”

Humphrey Polepole asikitishwa na Skizzy kuvamia, atoa kauli hii; “Tumepokea taarifa za kuvamiwa studio ya S2KIZZY ambako wasanii waliokuwa wakijiandaa kurekodi, wamepigwa na kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji. Haikubaliki! Tumesema na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio ili haki ipatikane na kuwachukulia hatua kali wavamizi. #Muzikinimaisha”

Click to comment
 
Blog Meets Brand