-->

Type something and hit enter

On
 RICHARD Djod, nyota wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa hawana hofu kwenye mchezo wao wa leo Oktoba 30 dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Azam FC ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 21 wanamenyana na JKT Tanzania yenye pointi 8 ikiwa nafasi ya 15 zote zimecheza mechi nane.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Mchezo uliopita kwa Azam FC ilifungwa kwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar inakutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kushinda mabao 6-1 dhidi ya Mwadui FC.


Djod mwenye bao moja na pasi moja ndani ya Azam FC ambayo imefunga mabao 14 amesema kuwa hawana mashaka kukutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kushinda mabao mengi kwenye mechi yao iliyopita.


"Hakuna mashaka kukutana na timu ambayo imefunga mabao mengi, ninaona kwamba wao wameshinda mabao 6-1 ilikuwa ni dhidi ya Mwadui na hawakutani na Mwadui kwa sasa wanakutana na Azam FC.


"Walikuwa kwenye uwanja mwingine kabisa na hapa wanakuja Uwanja wa Azam Complex hivyo kazi itakuwa ni mpya na sisi tunahitaji kupata ushindi," amesema.

Click to comment
 
Blog Meets Brand