-->

Type something and hit enter

On

MSANII wa kike wa Hip Hop kwenye muziki wa Bongo Fleva, Chemical ameomba ushauri wa kutaka msaada kwa sababu anajiona hana bahati kwani kila wanaume anayetaka kuwa naye kwenye mahusiano anamkataa.


Kupitia akaunti yake ya Instagram, Chemical ameaeleza; “Wana wa Insta, nipo hapa mbele yenu kuomba ushauri serious, nikisema nitajioa sio kwamba napenda, ila mwenzenu sina bahati jamani, nishatongoza sana ila wanaume msivyo na huruma hamuogopi kunikataa.

“Najua sivutii kihivyoo ila mgenihurumiapo basi, hata wa kuja na kupita tu au kunichezea nitaridhika, sasa sijui, niendelee kutongoza labda siku moja nitabahatika, ama nisubiri upepo wa kisulisuli au niachane na mapenzi nijioe na nizeeke na kibikra changu msaada wenu tafadhali,” amesema.
Click to comment
 
Blog Meets Brand