-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

UHONDO  wa Ligi kuu ya Uingereza (EPL) unaeendelea ikiwa mechi kubwa inayosubiriwa ni kati ya Manchester United ambao watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Old Trafford, kuwakaribisha matajiri wa jiji la London, Chelsea.

 

Timu zote zimeanza ligi vibaya na kazi kubwa hii leo kwa timu hizi ni kutafuta mwendelezo wa kushinda ili kuongeza ari kwa wachezaji wao.

 

Baada ya ushindi ugenini dhidi ya Paris Saint Germain (PSG) wa 2-1, United wanaingia na matumaini makubwa baada ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kuthibitisha kuwa mshambuliaji Edison Cavani yupo vizuri kucheza mechi hiyo baada ya kukosekana kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kurejea kwa wachezaji wake, Hakim Zeyich na Pulisic, kunampa kocha Frank Lampard uwanja mpana na kuchagua kikosi na mbinu za kutumia.  Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ule mzimu wa kushindwa kupata ushindi kwenye uwanja wa Old Trafford kwenye mechi sita mfululizo utaendelea leo ama la.

 

Chelsea wanaingia wakiwa wameshinda mechi mbili dhidi ya Brighton na Crystal Palace, wana sare mbili za magoli 3-3 dhidi ya West Bromwich Albion na Southampton,  na wamepoteza mechi moja nyumbani Stamford Bridge dhidi ya Liverpool.

Mashetani Wekundu wameshinda mechi zao sita kati ya saba lakini Old Trafford pamekuwa pachungu kwani bado hawajashinda mchezo wowote wakiwa wamepoteza mechi mbili  kwenye ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs na Brighton.

 

Ole Gunnar aliyeshinda mechi tatu kati ya nne anakutana Lampard, na swali lililopo ni, je: The Blues watachomoza na ushindi Old Trafford leo?

 

The post Chelsea Kuendeleza Uteja Kwa Mashetani Wekundu? appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand