-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

Hatimaye Mshambuliaji mpya wa timu ya Manchester United Edison Cavani ambaye alisajiliwa dakika za lala salama kutoka Paris Saint-Germain (PSG), ameanza mazoezi jana jumapili na kikosi cha kwanza baada ya kukamilisha wiki mbili za kujiweka  karantini nchini England.

Cavani ambaye analipwa Pauni laki 200,000 kwa wiki, amejumuishwa kwenye kikosi kitachosafiri kwenda Jijini Paris Ufaransa kuwavaa  waajiri wake wa zamani PSG, kwenye mechi ya ligi ya Mabigwa Ulaya kesho Jumanne sehemu ambayo alidumu kwa misimu saba tangu 2013-20 .

Fowadi huyo wa kimataifa wa Uruguay amesema, anatarajia yupo tayari kuipokea hali atakayo kutana nayo kwenye uwanja wa Stade de France  licha ya kutokuwa na mashabiki “nitakutana na hali tofauti pale lakini naamini itakuwa nzuri na kuvutia pia hasa pale unapokutana na timu yako ya zamani wengi hawakutarijia uhamisho huu ngoja tusubiri tuone”

United watakuwa ugenini kuwavaa PSG kwenye mchezo wa kundi H utakaopigwa kesho usiku, itakuwa mechi ya kulipa kisasi matajiri hao wa Jiji la Paris wakiingia na kumbukumbu ya kutupwa nje michuano hiyo msimu wa 2018-19 wakufugwa 3-1 na kuondolewa kwa faida ya goli la ugenini.

The post Cavani Aanza Mazoezi, Tayari Kuwavaa PSG appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand