Billinas: Nandy Anaanzaje Kuvua Pete Yangu! - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Billinas: Nandy Anaanzaje Kuvua Pete Yangu!


 MARA nyingi husemwa uhusiano wa kimapenzi wa mastaa ni wa tia maji tia maji huku wengi wakithibitisha kumwagana muda mfupi baada ya kudeti na kuwa wapenzi.

Sababu zinazotajwa ni kuwa “mafahari wawili hawawezi kuishi zizi moja”.

 

Lakini kwa msanii wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘ Billinass a.k.a Nenga na msanii mwenzie, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ kuna kauli tofauti kutoka kwao.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Billinass anasema yeye na mwanadada huyo ni mguu kwa mguu mpaka wafe wazikane.Amani Mtandaoni lilifanikiwa kukutana na msanii Billinas na kufanya naye mahojiano hasa baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba Nandy ameshavua pete yake ya uchumba.

 

AMANI:Mambo Billinas, vipi michongo inaendaje?

BILLINASS:Salama tu nashukuru Mungu, mambo yanaenda vizuri kila siku.

AMANI: Hongereni sana kwa NB, naona hadi bibie kakusifi a.

BILLINASS: Asante sana, unajua kwenye maisha lazima msukumane na kukumbushana ili vitu viende.Amani: Hivi kwako Nandy ana utofauti gani na wanawake wengine wengi uliowahi kuwa na uhusiano nao?

 

BILLINASS: Sitaki kumaanisha kuwa niwaponde wanawake niliowahi kuwa nao, lakini kwa kweli Nandy, amekuwa ni mwanamke wa pekee sana kwangu.

AMANI: Unaweza kuuelezea utofauti huo?

 

BILLINASS: Amekuwa ni mtu ambaye anajituma sana, robo tatu ya maisha yake ni mwanamke anayefanya kazi, muda mwingi sana anafi kiria maisha na ni mwanamke muelewa sana.

AMANI: Mbona kuna baadhi ya watu wanasema ni mkorofi , je umewezaje kukaa naye?

 

BILLINASS: Ni rahisi kusema hivyo, kwa sababu hawakai naye hata kidogo na wengine hawamjui kabisa, lakini ukweli ni kwamba ni mwanamke ambaye hapendi hata kidogo mambo ya ugomvi.

 

AMANI: Inadaiwa kuwa na wewe ni kama Uchebe, yaani ngumi mtu, unazungumziaje hilo?

 

BILLINASS: Siwezi kumpiga hata kidogo na sina mkono huo na hata ningekuwa napenda kupiga wanawake yeye nisingempiga kwa sababu ni mwanamke ambaye huwezi kuona kosa lake kirahisi.

 

AMANI: Mara nyingi tunaona uhusiano wa kimapenzi baina ya watu wanaofanya kazi moja ni ngumu hasa kwa upande wenu wanamuziki ni ngumu zaidi kudumu kwenye uhusiano unazungumziaje hilo?

BILLINASS: Kwa upande wangu au wetu ni ngumu hilo kutokea kabisa, tuna misingi mikubwa sana tumejiweke na kingine Nandy ni kama rafiki yangu, hivyo tunajuana na tunaweza kufanya mambo mengi bila tatizo.

 

AMANI: Mbona hivi karibuni ilionekana kama mlikuwa kwenye mgogoro na mpaka kuonekana Nandy, amevua pete ya uchumba uliyomvalisha?

 

BILLINASS: Unajua watu wanaweza kuona kitu alafu wanachukulia hivyo wanavyokiona, kwa sababu wanatamani kujua zaidi lakini wanashindwa, mimi sina shida kabisa na mpenzi wangu, inawezekana masikini alikuwa akipika au kuna jambo alikuwa anafanya, akavua lakini hakuna sababu kubwa ni hiyo tu na kingine hawezi kuvua pete yangu, ananipenda na mimi nampenda.

 

AMANI:Ungependa kuzaa watoto wangapi na Nandy?

 

BILLINASS: Mimi napenda sana watoto na yeye anajua kabisa, tumekubaliana tuzae watoto nane alafu ndiyo atapumzika.

 

AMANI:Inavyoonekana wazazi wa Nandy kama bado hawajakukubali vizuri, maana hawafunguki wazi kama wewe ni mkwe.

 

BILLNASS: Ni haki yao, kwa sababu siyo kila kitu wakiweke wazi kwenye mitandao ya kijamii, maana wale ni watu wazima na wanauelewa mkubwa, siku yenyewe ikifi ka wataweka wazi kila kitu.

 

AMANI: Nandy amekuwa anaandamwa sana na Gigy kwenye mitandao ya kijamii wewe kama mchumba wake unamwambiaje au kumshauri nini?

 

BILLINASS: Kila siku namuambia hauwezi kuwa na jina kubwa ushindwe kupitia mambo kama hayo, hivyo nampa moyo tu aendelee kupiga kazi.

 

AMANI: Ugomvi mwingi wa wapenzi unatokana na simu, kwa upande wako simu haijawahi kuleta shida kwenye uhusiano wenu?

 

BILLINASS: Hakuna kabisa na sisi kila mmoja anashika simu ya mwenzake muda wowote anaotaka, anajua namba yangu ya siri najua yake ndiyo maisha yetu.

 

AMANI: Unamwambia neno gani zuri, Nandy?

 

BILLINASS: Nataka kumwambia nampenda sana na nitaendelea kumpenda mpaka kufa kwangu .

 

AMANI: Haya shukrani sana.

 

BILLINASS: Asante sana

Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz