-->

Type something and hit enter

On
 KIKOSI cha Yanga kilicho nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 7 na kujikusanyia pointi 19 kitakutana na Biashara United iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo na 16 imecheza mechi 8.


Oktoba 31 Yanga ya Cedric Kaze ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United ya Francis Baraza mchezo utakaochezwa Uwanja wa Karume.

Msimu uliopita kwenye mchezo uliowakutanisha wapinzani hawa Uwanja wa Karume ngoma ilikuwa ni 0-0 hivyo kesho kazi itakuwa ngumu kwa timu zote kusaka rekodi mpya ndani ya uwanja huo.

Kaze amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na anaamini kwamba atapata pointi tatu muhimu.

"Mpaka sasa wachezaji wanazidi kuwa imara na imani yangu ni kwamba tutapata pointi tatu kwani nimeona namna kikosi kilivyo na muunganiko umeanza kupatikana,".

Baraza amesema kuwa anaamini kwamba anakutana na  timu yenye wachezaji wazuri na uzoefu lakini wachezaji wake wapo tayari kwa mchezo huo watapambana kusaka pointi tatu.

"Kila kitu kipo sawa wachezaji wapo tayari na ninaamini kwamba watafanya vizuri, wanajua wanakutana na timu yenye uzoefu ila hilo halitupi shida," . 

Click to comment
 
Blog Meets Brand