-->

Type something and hit enter

On
 BAADA ya kupokea vichapo kwenye mechi mbili mfululizo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamesema kuwa kwa sasa watapambana kutopoteza kwenye mechi zao zijazo ndani ya ligi ili wasifungwe.


Simba ilifungwa Oktoba 22 bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela na ilipoteza tena mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru kwa kufungwa bao 1-0.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ili kuweza kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa ni lazima wapate matokeo mazuri hivyo watapambana kwenye mechi zao zijazo.


"Bado nina amini kwamba Simba itatatwaa ubingwa kwa msimu wa 2020/21 lakini lazima tupate matokeo mazuri ambayo yatatupa pointi tatu muhimu.


"Kushindwa kwetu kwenye mechi zilizopita kunaleta maumivu hivyo mashabiki katika hili wanapaswa wajue kwamba tunahitaji jambo moja ambalo ni umoja na katika umoja wetu Simba hatujawahi kushindwa," amesema.


Kesho Oktoba 31, Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC Uwanja wa Uhuru.

Timu zote mbili zinakutana zikiwa zimetoka kupoteza mechi zao ambapo Mwadui FC wao wametoka kuchapwa mabao 6-1 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Mwadui Complex.

Click to comment
 
Blog Meets Brand