-->

Type something and hit enter

On
 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana kuendelea na rekodi ya kupata matokeo wakiwa Uwanja wa Azam Complex baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ilicheza mechi saba bila kupoteza ndani ya ligi ilikutana na balaa la Jaffary Kibaya wa Mtibwa Sugar aliyemtungua David Kissu dakika ya 62 akiwa nje ya 18.


Leo Oktoba 30 ina kibarua cha kumenyana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 15 na pointi 8 huku Azam FC ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake 21 zote zikiwa zimecheza mechi 8 ndani ya ligi.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kupoteza kwao mbele ya Mtibwa Sugar hakujawatoa kwenye reli watarudi kuendeleza rekodi yao mbele ya JKT Tanzania.

“Tumepoteza mbele ya Mtibwa Sugar hilo lipo wazi sasa kinachofuata ni kuendelea pale ambapo tulikuwa tumeishia kwa kusaka pointi tatu mbele ya JKT Tanzania kwani utakuwa mchezo wetu tukiwa nyumbani, mashabiki watupe sapoti,” amesema.


JKT mchezo wao uliopita walishinda mabao 6-1 dhidi ya Mwadui FC mchezo ambao uliweka rekodi ya kuwa mchezo wa kwanza kwa timu moja kufunga mabao mengi na hat trick ya kwanza ilipatikana kupitia kwa Adam Adam wa JKT Tanzania.

Click to comment
 
Blog Meets Brand