-->

Type something and hit enter

On
 ABDULKARIM Amin, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa wanahitaji kushinda mechi zao za mbele ikiwa ni pamoja na itakayochezwa kesho dhidi ya Mwadui FC kwa kuweka bayana kwamba wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo.


Tayari Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba imeshinda mechi tano ndani ya dakika 450 Oktoba 15 itashuka Uwanja wa Azam Complex kuwakabili Mwadui FC saa 1:00 Uwanja wa Azam Complex.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Azam FC imejikusanyia mabao 9 kwenye mechi nne na pointi zake ni 15 kibindoni ikiwa nafasi ya kwanza inakutana na Mwadui FC yenye pointi sita ikiwa nafasi ya nane.


Amin amesema:”Baada ya kushinda mechi zetu mbili ugenini mbele ya Mbeya City na Tanzania Prisons tumeweza kuona kwamba wachezaji wameongeza hali ya kujiamini na kuendelea na rekodi yao ya kupambana kushinda mechi za mbele.


"Kwa sasa ni kuona kwamba tunaweza kupata matokeo kwenye mechi zetu zinazofuata jambo ambalo lipo kwenye hesabu zetu na inawezekana kuendelea na rekodi hizo," amesema 


Ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo na mtupiaji namba moja ndani ya ligi anatoka Azam FC ni Prince Dube mwenye mabao matano na ametoa pasi mbili za mabao.

Click to comment
 
Blog Meets Brand