-->

Type something and hit enter

On
Msanii Barakah The Prince amemaliza utata uliokuwepo kati yake na msanii Alikiba na meneja Seven Mosha kwa kusema amewasamehe bure kwani hawawezi kumlipa kwa dhuluma walizomfanyia.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Barakah The Prince amesema ameamua kusamehe, kusahau na kutofuatilia yaliyotokea japo anaamini waajiri wake wa zamani bado wana kinyongo naye.


"Naomba leo tufunge mjadala wa Alikiba na Seven Mosha, sina noma na mtu yeyote labda wao ndiyo wana noma na mimi nimezika na nimefukia muda mrefu sana maana hawawezi kuwa na pesa ya kunilipa kwenye kipaji changu kama nikiamua kufuatilia kutokana na dhuluma na vitu vyote walionifanyia, nitakuwa namuonea tu" amesema Barakah The Prince 


Barakah The Prince alisainiwa Rockstar4000 mwaka 2016 chini ya Mkurugenzi na meneja lebo hiyo Seven Mosha na msanii Alikiba ambaye ni mshirika wa kampuni hiyo kwa upande Afrika Mashariki.Click to comment
 
Blog Meets Brand