-->

Type something and hit enter

On
 BEKI wa zamani wa Simba ambaye anakipiga ndani ya Highland Parks FC ya nchini Afrika Kusini, Abdi Banda amerejea nchini kwa mapumziko mafupi baada ya timu yake kuuzwa na kubadilishwa jina na kuitwa Ts Galaxy.

 

Akizungumza na Saleh Jembe Banda amesema kuwa mwisho wa mwezi wa kumi alipigiwa simu na uongozi wa timu ya Ts Galaxy, ili waweze kumtumia tiketi lakini wakala Keegan Wasser raia wa Uingereza alimkataza.


“Nipo likizo lakini pia natumia muda wangu kutafakari ni wapi nitaenda sababu timu yangu iliuzwa kutoka Highlands Parks FC mpaka sasa inaitwa Ts Galaxy.

 

“Bosi wa timu mpya alinipigia simu mwezi huu mapema kutaka kunitumia tiketi ili niweze kurejea kujiandaa na ligi ila wakala wangu alikataa kwani alitakiwa kuzungumza naye kwanza juu ya mkataba wa miaka miwili uliobaki ambao nilikuwa niutumikie nikiwa Highland.


"Kwangu mimi ninajua kwamba mambo yatakwenda sawa na mazungumzo yakienda sawa nitarejea Afrika Kusini kuendelea na kazi yangu ila kwa sasa nitasubiri kwanza ili nijue mambo yatakwendaje," amesema Banda.

Click to comment
 
Blog Meets Brand