-->

Type something and hit enter

On
  Manchester United haijakata tamaa katika mbio zao za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Uingereza Jadon Sancho, 20. (ESPN)

Tottenham inafikiria kumchukua tena mlinzi wa Inter na Slovakia Milan Skriniar, 25, lakini haiko tayari kumsajili kwa bei yake. (Guardian)

Barcelona inakaribia kufikia makubaliano ya mwisho na Ajax kuhusu beki wa kulia wa Marekani Sergino Dest, 19, lakini ina uwezo mdogo wa kufanya makubaliano zaidi ya usajili. (Goal)

Manchester United itamruhusu winga raia wa Wales Daniel James, kujiunga na Leeds United kwa mkopo, lakini kama watamsajili Sancho. (Sun)


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Everton na Leicester City zote zinamnyatia mlinzi wa Chelsea raia wa Ufaransa Kurt Zouma, 25. (Le10 Sport, via Talksport)

Sheffield United imetoa ofa kwa Liverpool ya pauni milioni 17 kwa mshambuliaji wa England wa Under-21 Rhian Brewster na iko tayari kujumuisha kipengele cha kumnunua kwenye makubaliano. (Sun)

Bayern Munich inafikiria kutoa ofa kwa beki wa kulia wa Norwich City Max Aarons, 20.

Kocha wa Everton Carlo Ancelotti hatarajii kuwa winga Theo Walcott, 31, ataondoka katika klabu hiyo kipindi hiki cha usajili. (Mail)

Lazio inafanya mazungumzo kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Brazil Andreas Pereira, 24, kwa kipindi kirefu kwa mkopo kukiwa na chaguo la kumnunua. (Telegraph)

Mlinzi wa Tottenham na Argentina Juan Foyth, 22, ndio mlengwa wa Valencia. (COPE - in Spanish)

Leeds United iko katika hatua ya mwisho ya majadiliano na Bayern Munich kuhusu kiungo wa kati Mickael Cuisance, 21, baada ya raia huyo wa Ufaransa kuiarifu klabu yake ya Ujerumani kuwa anataka kuingia kwenye kikosi cha wachezaji mara kwa mara. (Sport Bible, via Fabrizio Romano)

Lyon iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa, 22, Houssem Aouar, ambaye anahusishwa na kuhamia Arsenal

Click to comment
 
Blog Meets Brand