SVEN AWAPA MBINU MPYA WACHEZAJI WAKE KUIMALIZA BIASHARA UNITED - EDUSPORTSTZ

Latest

SVEN AWAPA MBINU MPYA WACHEZAJI WAKE KUIMALIZA BIASHARA UNITED


 KIKOSI cha Simba, leo Septemba 20 kitakuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa jijini Dar kupambana na Biashara United.


Mchezo wa leo ni wa kwanza kwa Simba kucheza nyumbani ambapo ilicheza mechi mbili za ligi kwa msimu wa 2020/21 ikiwa ugenini.

 Katika mechi mbili za ugenini, ilianza kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, mechi iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Baada ya hapo, ikalazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Kwa upande wa Biashara, inaingia uwanjani leo ikiwa na ushindi wa asilimia 100 kutokana na kushinda mechi zote mbili nyumbani kwenye Uwanja wa Karume, Mara kwa matokeo ya 1-0 dhidi ya Gwambina na Mwadui.

 

Simba ikiwa imeruhusu mabao mawili kwenye mechi mbili, leo ina kazi kubwa ya kuipenya ngome ya Biashara ambayo katika mechi hizo, haijaruhusu bao.

 

Katika hilo, Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck, amewakabidhi majukumu mazito mawinga wake, Bernard Morrison na Luis Miquissone ya kuhakikisha wanaipenya ngome ya Biashara na kupata ushindi.


Sven katika mazoezi ya mwisho kabla ya leo kucheza na Biashara, alikuwa akiwapatia mbinu za umaliziaji na kupiga mashuti nje ya 18 wachezaji wake wote ambapo mawinga hao walifanya kwa ustadi mkubwa.


Kocha wa Biashara United, Francis Baraza raia wa Kenya, amesema: “Tunaifahamu Simba ni timu kubwa, tangu msimu uliopita walikuwa na kikosi bora na msimu huu pia wamefanya usajili kwa kuwaongeza wachezaji wengine bora, hivyo natarajia tutakuwa na mchezo mzuri na mgumu.

 

“Licha ya kuwapa heshima kutokana na ukweli kwamba wao ndiyo mabingwa watetezi, lakini hatutawaogopa, tutajitahidi kucheza tukiwa na lengo la kusaka pointi tatu kwa kuwa tunao uwezo huo.”

 

REKODI


Huu ukiwa ni msimu wa tatu kwa Biashara United ndani ya Ligi Kuu Bara, imekutana na Simba mara nne.Katika mechi hizo, Simba imeshinda tatu na sare moja.

 

Haijapoteza, huku Biashara ikishindwa kupata ushindi mbele ya Simba.Mbali ya kushindwa kupata ushindi mbele ya Simba, pia Biashara haijaambulia ushindi wowote ilipotua Dar kucheza mechi ya ligi ikiwa imecheza Dar mara tisa. Ushindi wao mkubwa ni sare ambapo imezipata tatu na kupoteza mechi sita.

Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.