-->

Type something and hit enter

By OnKLABU ya Simba, imezifunika timu nyingi Afrika ikiwemo Al Ahly na Zamalek, kutokana na kushika namba moja kwa umaarufu zaidi kwenye Mtandao wa Instagram.

Hiyo ni kwa mujibu wa Mtandao wa Deporfinanzas ambao umetoa takwimu za Mwezi Agosti na kuiweka Simba namba moja kwa umaarufu kutokana na kutembelewa sana na watu.Takwimu zinaonesha kuwa, kwa mwezi huo, watu milioni 536 walitembelea akaunti hiyo ya Simba, huku Al Ahly ya Misri ikiwa na milioni 517 na Raja Casablanca ya Morocco ikiwa na milioni 511.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Mtandao huo uliandika hivi: “Simba SC ndiyo klabu maarufu Afrika ndani ya Instagram kwa mwezi Agosti 2020!“Hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka Tanzania kufanya hivi.”Baada ya kutoka takwimu hizo, Simba nao waliposti taarifa hiyo kwenye mitandao yao ya kijamii kwa kuandika: “Uwanjani 100%, mitandaoni 100% na pia chapa kubwa, weka mbali na watoto.”

Mapema wiki hii, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mulamu Nghambi, wamekuwa na ziara nchini Misri ambapo walianza kutembelea Klabu ya Al Ahly, kisha jana walitembelea Zamalek.

 

Baada ya kutembelea klabu hizo, walipata nafasi ya kukutana na viongozi wa klabu hizo ambapo wamekubaliana kushirikiana katika mambo mbalimbali ambayo yataisaidia Simba.

ULIUS RICHARD, Dar

JULIUS RICHARD, Dar

The post Simba Yaipiga Bao Al Ahly Kwenye Mtandao appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand