-->

Type something and hit enter

On
 UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo Septemba 28 utaanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania. 


Simba itakuwa ugenini Oktoba 4, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo itamenyana na JKT Tanzania.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa leo wataanza na mazoezi ya Gym kisha jioni watafanya mazoezi Uwanja wa Bunju.


"Tumetoka kushinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC,  program ya Kwanza ilikuwa mapumziko jana na leo asubuhi mazoezi ya Gym na jioni tutakuwa Uwanja wa  Bunju.


"Kikubwa tunahitaji kuendelea kupata matokeo Kwenye mechi zetu na mchezo wetu ujao itakuwa ni dhidi ya JKT Tanzania, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema. 


Simba imetoka kushinda mbele ya Gwambina Uwanja wa Mkapa inakutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union.

Click to comment
 
Blog Meets Brand