-->

Type something and hit enter

On
 SIMBA leo wameanza mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Oktoba 4 Uwanja wa Jamhuri Dodoma dhidi ya JKT Tanzania.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kikosi kipo sawa na kinaendelea na programu za mwalimu ili kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


"Leo tumeanza na mazoezi maalumu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania, nina amini kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini kwa kuwa sisi ni mabingwa lazima tujipange sawasawa.

"Kwa upande wa benchi la ufundi baada ya kutoka kushinda mbele ya Gwambina FC wao pia wapo sawa wanatambua kwamba mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania utakuwa na ushindani mkubwa, mashabiki watupe sapoti," amesema.


JKT Tanzania itamenyana na Simba ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Click to comment
 
Blog Meets Brand