-->

Type something and hit enter

By OnBAADA ya Prince Dube kuifungia Azam FC bao la ushindi dhidi ya Tanzania Prisons ni wazi nyota huyo anakula sahani moja na washambuliaji kama Meddie Kagere na Chris Mugalu, ambao wamekuwa na uwiano mzuri wa kufunga.


 Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Dube tangia asajiliwe na Azam amekuwa na kiwango kizuri hususani katika michezo ya ligi kuu mara baada ya kufanikiwa kufunga mabao matatu na kutoa pasi ya bao moja katika michezo minne aliyoichezea timu hiyo.

Dube katika michezo hiyo minne aliyoichezea Azam alifanikiwa kufunga katika michezo miwili dhidi ya Coastal Union alipofunga mabao mawili kisha akafunga bao moja katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Michezo mingine ni dhidi ya Polisi Tanzania ambapo alitoa pasi ya bao lililofungwa na Obrey Chirwa huku katika mchezo dhidi Mbeya akishindwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.

 

Baada ya kufunga mabao hayo matatu kwenye ligi, Dube ni wazi anakula sahani moja na washambuliaji wengine kama Meddie Kagere na Chris Mugalu wa Simba ambao wamefunga mabao mawili kila mmoja.

The post Prince Dube Ala Sahani Moja na Kagere, Mugalu appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand