-->

Type something and hit enter

On  


Wanasemaga mapenzi sio pesa ila pesa hiyohiyo ikikosekana mapenzi yanapungua, lakini msemo huo umekuwa tofauti na mtangazaji Bhoke Egina ambaye amesema akimpenda mwanaume kwenye mahusiano hana shida ya pesa kwani hata yeye mwenyewe anazo.

Bhoke amesema hilo kwenye show ya Dadaz ya East Africa Tv ambapo amenukuliwa akisema  "Mimi nikikupenda sijali wala siombi pesa kwanza nina kila kitu, nikiwa na Mwanaume nataka ajue kwamba nimempenda kutoka moyoni" 

Sasa mara baada ya kusema hivyo amezua mijadala kwa watumiaji wa mtandao wa Twitter ambapo wame-comment kuhusu alichokisema kwa kuandika kuwa 

"Maneno haya usemwa na wadada wengi walioko single" Craldo 19 

Vizuri" Excellence Management 

"Kipo anachotaka japo ana kila kitu" Kzg Kzg 200 

"Mimi nataka niwe naye" Ally Hussein A Town 

Hizo ni comment za baadhi ya watu waliotoa maoni yao kuhusu alichokisema Bhoke kwenye show ya Dadaz siku ya Leo Septemba 17, 2020.Click to comment
 
Blog Meets Brand