-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BIG bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia ameibuka na kumkingia kifua straika wake, Yacouba Songne kwa kusema kuwa anahitaji muda kwa ajili ya kuonyesha uwezo wake.

 

Mserbia huyo ameongeza kuwa kwa sasa straika wake huyo anaendelea kuwa sawa kutokana na kukaa zaidi ya miezi mitano bila ya kucheza mpira kutokana na suala la virusi vya Corona.

Yacouba ambaye amesajiliwa na Yanga akitokea Asante Kotoko ya Ghana hadi sasa ameshacheza mechi mbili akiwa na klabu hiyo dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons huku akishindwa kufunga bao lolote.

 

Krmpotic ameliambia Championi Ijumaa, kuwa hawezi kumlaumu straika huyo kwa kushindwa kufunga katika mechi hizo kwa sababu ya kukaa muda mrefu bila ya kucheza kutokana na ligi yao kusimama kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.

 

“Yacouba hajacheza kwa miezi mitano iliyopita kwa sababu ya Corona, siyo rahisi kuonyesha kiwango kikubwa kwa kipindi hiki ambacho anacheza kwa sasa.

 

“Lakini pia amefika hapa wiki chache nyuma ndiyo akaanza mazoezi na wenzake. Namuandaa kuja kuwa hatari kwa siku zijazo pale ambapo atakaa sawa na kuelewana na wenzake ndani ya timu,” alimaliza Mserbia huyo.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

ALICHOJIBU Kocha SIMBA kuhusu KAGERE Kukaa BENCHI – “NITA DISCUSS Nae YEYE”

The post Mserbia Yanga SC Amkingia Kifua Straika Mburkina Faso appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand