Mfahamu Muigizaji wa Marekani Leonardo DiCaprio | EDUSPORTSTZ -->

Type something and hit enter

OnPakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


 Novemba 11, 1974 alizaliwa mwigizaji, prodyuza na mwanamazingira wa nchini Marekani Leonardo DiCaprio.


Ametunukiwa tuzo mbalimbali zikiwamo tatu za Golden Globe. DiCaprio alizaliwa jijini Los Angeles akiwa ni mtoto pekee wa Irmelin ambaye alikuwa katibu wa sheria na baba yake George DiCaprio ambaye alikuwa mwandishi, mchapishaji na msambazaji wa vitabu vya vikaragosi. Baba yake ni wa uzao kutoka Italia na Ujerumani. Katika mojawapo ya mahojiano DiCaprio aliwahi kusema yeye ni nusu raia wa Russia kutokana na mababu zake wawili waliopita walitokea nchini Russia.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Wazazi wake walikutana Los Angeles walipokuwa masomoni. DiCaprio alipewa jina la Leonardo kwasababu wakati akikaribia kujifungua mama yake alikuwa akingalia michoro ya mchoraji maarufu duniani Leonardo da Vinci katika makumbusho ya Ufizi mjini Florence nchini Italia.

Nyota huyo mwaka huu amekusanya kiasi cha dola za kimarekani bilioni 7.2 katika mauzo ya filamu. Mapato hayo yamemweka katika nafasi ya nane ya waigizaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha wa zama zote.

DiCaprio ameonekana katika filamu nyingi ikiwamo ya This Boy’s Life. Mwaka huu wa 2019 ameonekana katika filamu ya Once Upon a Time in Hollywood. Mnamo mwaka 2016 alitajwa na jarida la TIME kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi duniani.
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment
 
Blog Meets Brand