-->

Type something and hit enter

On
 DAR: Memba mwingine wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mbwana Yusuf ‘Mbosso Khan’ ameingia kwenye tuhuma nzito ya wizi wa mashairi kama ilivyotokea kwa msanii Zuhura Othman ‘Zuchu’.

 

Mbosso anatuhumiwa kukopi mistari ya mtu na kuiweka kwenye wimbo wake mpya wa Sina Nyota.Wiki moja baada ya wimbo huo kuteka pale mjini YouTube na kutazamwa mara zaidi ya milioni 2, dogo mmoja ameibuka na tuhuma hiyo nzito dhidi ya Mbosso, ambaye anaaminika kuwa ni mtunzi mahiri wa nyimbo za kubembeleza, zenye mahadhi ya pwani.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Dogo huyo anayejiita Dach Boy, anadai kuwa, kwenye wimbo huo wa Mbosso, kuna mashairi ya wimbo wake wa Tete.

 

Kwa mujibu wa Mtandao wa YouTube, wimbo huo wa Tete uliachiwa wiki tatu zilizopita, ukiwa na mashairi yanayosema; “Ila najua bado nipo, ila hali yangu hoehae…sina mabadiliko…machozi mafuriko fundi wa jiko langu akaacha mawe akalamba mwiko.”

 

Katika hali ya kushangaza, wimbo wa Mbosso nao una mashairi hayohayo isipokuwa utofauti upo kwenye ala, melodi na mwimbaji.

 

Wakati wimbo huo wa Mbosso ukitazamwa zaidi ya mara milioni 2, ule wa Dach Boy, wenyewe umetazamwa mara zaidi ya 800!Hata hivyo, nyimbo zote zinazungumzia mapenzi.

 

Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Mbosso ili kujibu madai hayo, lakini alisema yupo bize na kwamba, alielezwa juu ya tuhuma hizo ambazo zimekuja sambamba na nyingine za Tanasha Donna dhidi ya Zuchu, anayedaiwa kutumia mashairi ya wimbo wa Ride wa Tanasha kwenye wimbo wake wa Cheche akiwa na bosi wake, Diamond Platnumz.

Dach Boy ni msanii mchanga anayechipukia kwenye Bongo Fleva.

Click to comment
 
Blog Meets Brand