-->

Type something and hit enter

On
 KLABU ya Liverpool imethibitisha kuwa imepata saini ya nyota wa Bayern Munich, Thiago Alcantara kwa dili la miaka minne.

Kiungo huyo raia wa Hispania kwa sasa atakuwa ni mali ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England ambao waliutwaa msimu uliopita baada ya miaka 30 kumeguka.

Thamani ya nyota huyo inatajwa kuwa pauni milioni 25 na Liverpool imefikia makubaliano mazuri na mabingwa hao wa Ujerumani hivyo msimu huu wa 2020/21 atakuwa ndani ya Anfield.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Thiago amesema:"Nadhani ni maajabu kwangu ndizo hisia ambazo ninazo. Nilisubiri kwa muda mrefu hatimaye imeweza kutimia, nina furaha kubwa kuwa hapa.

"Kadri muda unayokwenda unatamani kushinda zaidi na ukishinda unahitaji kushinda tena zaidi. Ninafikiria kwamba klabu ina malengo makubwa nami pia ninahitaji kufikia mafanikio hayo na kushinda mataji zaidi."

Click to comment
 
Blog Meets Brand