-->

Type something and hit enter

On
 YANGA SC kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Eng. Hersi Said, wamethibitisha kuwa Beki wao wa kimataifa  Mghana Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuichezea Yanga hadi 2023.


Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuwatumikia mabosi wake Yanga hadi mwaka 2023.

Lamine, raia wa Ghana hivi karibuni iriripotiwa kuwa mkataba wake unakaribia kufika ukingoni jambo ambalo limewafanya mabosi wake kumpa dili jipya kutokana na uwezo wake kuwa ndani ya uwanja.

Lamine amesema:-"Ni kweli nimeona vyema kuongeza mkataba, kwanza itanipa  muda zaidi wa kutekeleza majukumu yangu."

Beki huyo kisiki alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bidcom ya Zambia mkataba  ambao unamalizika mwishoni mwa msimu ujao. Lamine ataendelea kubaki mitaa ya Jangwani  hadi Julai 2023.
Ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa amecheza mechi tatu na amefunga mabao mawili.

Click to comment
 
Blog Meets Brand