-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BEKI wa Yanga, Lamine Moro, amefunguka kuwa kama kiungo wa timu hiyo, Carlos Carlinhos, ataendelea kupata nafasi ya kucheza, basi yeye atakuwa anafunga sana kwa kuwa ni mtu ambaye anamjulia.Lamine Moro amefunga mabao mawili, ndani ya dakika 270 alizocheza ambazo ni sawa na michezo mitatu.

 

Alifunga bao pekee kwa Yanga kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City uliochezwa Mkapa, Dar kisha akafanya hivyo pale Jamhuri dhidi ya Mtibwa na mabao yote ni ya kona zilizochongwa na Carlinhos.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Lamine alisema, Carlinhos ni mchezaji mzuri sana kwenye mipira ya kona na faulo, lakini jambo zuri zaidi anafahamu namna ya kupiga mipira ambayo inaipa faida timu, hivyo kama mchezaji huyo atadumu kwenye kikosi cha Yanga basi atakuwa anafunga sana.

“Carlinhos Mungu amempa kipaji kikubwa cha kucheza mipira iliyokufa, anajua kuchonga kona na kupiga faulo nzuri na zenye malengo. Kama ataendelea kuwa vile, mimi naweza kusema nitafunga sana msimu huu,” alisema Lamine.

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam

MAADHIMISHO ya SIKU ya KANSA DUNIANI, WADAU Wajitokeza KUWAFARIJI WAGONJWA

The post Lamine Moro Aahidi Makubwa Yanga SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand