Kagere Ndiyo Basi Tena Simba-Michezoni leo | EDUSPORTSTZ -->

Type something and hit enter

By OnPakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

NDIYO basi tena! Ndivyo utakavyoweza kusema kwa mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere ni baada ya kocha wake Mserbia, Sven Vandenbroeck kutoa kauli ya kumkatisha tamaa mfungaji bora huyo mara mbili mfululizo.

 

Kagere ambaye misimu miwili alitwaa ufungaji bora msimu wa 2018/2019 akitupia mabao 23 na 2019/2020 akifunga mabao 22 hivi sasa ameonekana hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichochukua ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo.


 Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Kocha huyo alionekana kuanza kupoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kwenye msimu uliopita kutokana na mfumo ambao Mbelgiji huyo amekuwa akiutumia wa 4-5-1 ukihitaji mshambuliaji mmoja ambaye hivi karibuni alimtaja nahodha wake, John Bocco ndiye anayeumudu kucheza katika kikosi chake.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Sven alisema mshambuliaji huyo kuwa mfungaji bora misimu miwili akifunga mabao 45 siyo sababu ya kumpanga kucheza katika kikosi chake cha kwanza.

Sven alisema kuwa yupo mshambuliaji kutoka nchini Italia (Ciro Immobile anayeichezea Lazio, Italia) ametwaa ufungaji bora mara mbili ambaye yeye msimu mmoja alifikisha mabao 32.

 

Aliongeza kuwa kama mshambuliaji huyo raia wa Italia amekuwa mfungaji bora kwa kufunga mabao 32 anakaa benchi itakuwa kwa Kagere aliyefunga 20.

 

“Kama mfungaji bora misimu miwili wa Ligi Kuu ya Italia anakaa, straika (Immobile) ambaye yeye aliwahi kufunga mabao 32 anaanzia benchi itakuwa kwa Kagere aliyefunga 20.

 

“Hilo suala la kukaa benchi naomba mniachie mimi, nitakwenda kukaa naye na kuzungumza naye kwani hilo suala la binafsi lipo ndani ya timu siyo la kuzungumza,” alisema Sven.

 

Kocha huyo hivi karibuni aliweka wazi juu na hatma yake ya kucheza katika kikosi cha kwanza kwa kutamka kuwa: “Kagere hana nafasi ya kucheza katika kikosi changu, Bocco ndiye mwenye nafasi hiyo ni kutokana na kiwango bora ambacho amekuwa akikionyesha.”

Stori: Wilbert Molandi, Dares Salaam

ALICHOJIBU Kocha SIMBA kuhusu KAGERE Kukaa BENCHI – “NITA DISCUSS Naye YEYE”

The post Kagere Ndiyo Basi Tena Simba appeared first on Global Publishers.Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment
 
Blog Meets Brand