-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MMOJA wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Zacharia Hans Poppe, kama ameimpa mechi 10 tu timu ya Yanga ambayo inatamba na kiungo mshambuliaji wao, Carlos Carlinhos.

 

Carlinhos ni kati ya wachezaji gumzo hapa nchini kwa sasa akiwa amefanikiwa kutoa pasi moja ya bao kwenye mchezo mmoja wa ligi aliocheza akiingia akitokea benchi.

 

Wikiendi iliyopita alikuwa gumzo baada ya kuisaidia timu yake ya Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Championi Jumatano, Hans Poppe amesema ni mapema mno kuweza kuzungumzia viwango vya timu na wachezaji kwa sasa kwa kuwa hazikwenda katika maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’.

“Ligi ni ngumu kila timu inahitaji kuona inafanikiwa kufanya vyema huko mbele, lakini ni mapema mno kuweza kutoa tathimini ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwani hakuna ambayo ilikwenda kufanya Pre Season kwa kuwa muda ulikuwa hautoshi.

“Hivyo ni mapema mno kuelewa itakuwaje na nani staa kwa sasa hadi mechi ya 10 huko ndio timu zitaanza kuwa na ushindani na itafahamika nani ni staa na timu gani ni bora, kwa sasa ndiyo maana timu nyingi hazifanyi vizuri,” alisema Hans Poppe.

Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam

UCHAMBUZI: SARE ya SIMBA vs MTIBWA SUGAR, USHINDI wa YANGA dhidi ya MBEYA CITY

The post Hans Poppe Awapa Yanga Mechi Kumi appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand