-->

Type something and hit enter

On
MCHEZO kati ya Mtibwa Sugar na Simba Uwanja wa Jamhuri, Morogoro umekamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1.

Simba ilianza kupachika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Mzamiru Yassin dakika ya 45. Mtibwa Sugar waliweka usawa dakika ya 46 kupitia Boban Ziringitus kwa kichwa akiwa amezungukwa na msitu wa mabeki wa Simba.

Huu ni mchezo wa pili kwa timu zote mbili ndani ya msimu mpya wa 2020/21 ambapo mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 2-1 mbele ya Ihefu na leo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar.


 Mtibwa Sugar mchezo wao wa kwanza walilazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Ruvu Shooting na leo wamelazimisha sare ya bila kufungana na Simba, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Click to comment
 
Blog Meets Brand