-->

Type something and hit enter

On

Nyota wa Bongo Diamond Platnumz ni msanii ambaye anaogopwa sana Afrika Mashariki katika masuala ya wanawake.


Diamond amehusishwa kimapenzi na vipusa wengi tangu nyota yake katika fani ya muziki ilipoanza kung'aa.Diamond alizua mdahalo mitandaoni baada ya kuelezea hisia zake kumhusu dadake msani Vanessa Mdee, Mimi Mars.


Alipakia video fupi ya kipusa huyo akiufurahia wimbo wake wa Cheche ambao alimshirikisha Zuchu, na kutokana na ujumbe aliouchapisha chini ye video hiyo ni bayana vitu vitamu havimpiti.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Baba huyo wa watoto wanne alikiri kwamba anampenda kidosho huyo na hata kusema hajui ni kwa nini hajawahi kuwa na uhusiano wa mapenzi naye.


"Nimekuwa nikimpenda mrembo huyu. Sijui kweli nilikuwa wapi mimi mtoto wa Mama Dangote. Doh! @ Mimi_mvrs11," aliandika Diamond.


Wajuzi wa mitandaoni walimiminika kwenye ukurasa wake Diamond na kutoa maoni yao kuhusu ujumbe wa nyota huyo.


Wengi wao walimuuliza msanii huyo toka Tanzania endapo yuko tayari kuchumbiana na mrembo mwingine baada ya uhusiano wake na Tanasha kufeli.


Aishasiku alisema: "Lo! Unataka sasa kurejea Tanzania? Naona bado hujamalizana na Burundi na Rwanda.


Mwingine aliyetambulika kama _.flawless.chica_ alimtaja Diamond kama simba ambaye anayependa minofu ya binadamu.Mbali na hayo Diamond amezidi kudhihirisha kwamba yeye ni staa wa kutajika ambaye amewahi ibuka Afrika Mashariki.


Hii ni baada ya kushirikiana na mwimbaji maarufu wa midundo ya RnB Alicia Keys kwenye albamu yake mpya.


Diamond alishirikishwa katika wimbo wake Alicia unaoitwa Wasted Energy.


Hii ni kama heshima ya msanii huyo wa wimbo maarufu wa Jeje kwani ni yeye mwimbaji pekee Afrika amewahi shirikishwa kwenye albamu hiyo.

Click to comment
 
Blog Meets Brand