-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BONDIA wa Tanzania, Cosmas Cheka, ameshinda pambano dhidi ya Mmalawi, Hannock Phiri, lililofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2020.

Mabondia hao walipigana Kwa uzito wa Light kuwania UBO International Title ambapo pambano hilo lilikuwa la round 12.

Kwa uamuzi wa majaji, ameonekana kushinda japo mpinzani wake ameonekana kutokubaliana na uamuzi huo wa kupoteza pigano hilo.

Mbali na hayo, Cheka amesema kuwa kama mpinzani wake hajaridhika, arudie pambano na kwamba yeye yuko tayari kumfuata Malawi.

Katika Mapambano ya utangulizi, Mwanadada Zulfa Macho, mtoto wa Yusuph Macho alishinda kwa knock-out kwenye raundi ya kwanza kwenye pambano dhidi ya Mmalawi, Ndau Chilimba.

The post Cheka Amtwanga Mmalawi, Atwaa Ubingwa wa UBO appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand