-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos raia wa Angola, amevunja ukimya kwa kusema kuwa anaamini timu hiyo itafikia malengo ndani ya msimu huu licha ya kuanza kwa kusuasua.

 

Yanga imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara ikiwa imeshinda moja na kutoka sare moja jana timu hiyo iliondoka kwenda Kagera kuumana na Kagera Sugar.

 

Kiungo huyo amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Petro Luanda ya nchini kwao Angola na ameanza vizuri katika ligi kuu baada ya kucheza mechi yake ya kwanza kwa dakika 29 dhidi ya Mbeya City akiwa ametoa pasi moja ya bao huku akiwa amepiga kona tano.

Carinhos ametoa kauli hiyo kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram baada ya mchezo wa kirafiki wa juzi Jumatano dhidi ya Mlandege ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

 

“Mazoezi yalikuwa mazuri, tutafika hatua kwa hatua na tutaweza kufikia malengo yetu,” aliandika kiungo huyo.

Stori na Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

The post Carlinhos Atoa Kauli ya Matumaini Yanga appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand