BWALYA APEWA MAJUKUMU MENGINE NDANI YA SIMBA - EDUSPORTSTZ

Latest


 

BWALYA APEWA MAJUKUMU MENGINE NDANI YA SIMBA


 BOSI wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, amembebesha majukumu mazito kiungo wake Mzambia Rarry Bwalya la kuhakikisha anaonyesha kiwango kwenye mechi zao za ugenini baada ya kung’ara kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Kocha huyo amempa majukumu Bwalya na wachezaji wengine wa kikosi hicho kuhakikisha wanaonyesha uwezo mkubwa katika mechi zao za mkoani kwa ajili ya kuipa timu hiyo matokeo.


Bwalya amekuwa mmoja wa viungo walioonyesha ufundi katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Gwambina ambayo alianza na Biashara United Uwanja wa Mkapa, Dar.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Simba watacheza mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara Oktoba 4, dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Mbelgiji huyo amesema kuwa anataka kuwaona wachezaji wake wote wakicheza kwa kiwango kikubwa kutokana na wengi kuwa na uwezo mkubwa.

 

“Wiki ijayo tunatoka kwenda ugenini dhidi ya JKT Tanzania, natarajia tutacheza hivihivi kwa kiwango kizuri hata kama kiufundi hatutacheza kama mechi iliyopita dhidi ya Gwambina.

 

“Lakini natarajia tunatakiwa kupambana kwa nguvu kama mechi zetu mbili zilizopita na uzuri ni kuwa tuna watu wengi wa kufunga mabao.”


Bwalya alijiunga na Simba kwenye usajili huu akitokea Power Dynamos ya Zambia.Kwenye mchezo dhidi ya Gwambina alisababisha faulo iliyofungwa na Pascal Wawa.


Inakutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz