-->

Type something and hit enter

By OnOFISA Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez,  leo Septemba 24, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika, Ahmad Ahmad,  kwenye makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo jijini Cairo, Misri.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Baada ya kukutana,  Ahmad amempongeza Barbara kwa kupata nafasi hiyo kubwa, lakini pia kumtaka kuitumia vyema ili kuonyesha kwamba anaimudu kazi hiyo ambapo itakuwa ni moja ya njia ya kuhamasisha wanawake wengine kushika nafasi za juu za uongozi wa soka.

 

Kwa upande wake Barbara amemshukuru Ahmad na CAF kwa mapokezi mazuri, lakini pia kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia kukuza soka la Afrika.

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa CAF, Abdelmounaïm Bah, Makamu Katibu Mkuu wa CAF, Anthony Baffoe na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi.

   

The post Bosi Simba Akutana na Rais wa CAF Cairo, Misri appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand