-->

Type something and hit enter

By On



Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MSHAMBULIAJI na nahodha wa Simba, John Bocco amesema kuwa huu utakuwa msimu mgumu kwao kwenye Ligi Kuu Bara kutokana na kila timu kuwapania lakini watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

 

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

 

Simba katika mechi ya kwanza msimu huu ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu kabla ya kubanwa mbavu na Mtibwa.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Bocco alisema kuwa kitendo cha wao kuchukua ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo ndiyo kumesababisha wapaniwe na kila timu.

 

Bocco alisema kuwa kupaniwa huko hakutawafanya wao kupata matokeo mabaya kwenye michezo ijayo na badala yake watahakikisha wanapambana ili wapate ushindi kwa lengo la kulitetea taji lao.

 

“Kwanza tunashukuru kumaliza mchezo wetu dhidi ya Mtibwa salama kukiwa hakuna majeruhi yeyote, hivyo hivi sasa tunaelekeza nguvu kwenye mchezo ujao ili kuhakikisha tunapata ushindi baada ya sare dhidi ya Mtibwa.

 

“Kiukweli mechi haikuwa nyepesi kutokana na kila timu kupania kuhakikisha wanapata matokeo mazuri, wachezaji tumeumizwa na matokeo ya sare ambayo hayakuwa malengo yetu.

 

“Hivyo, tunajipanga kwa ajili ya michezo ijayo, kikubwa ni kuhakikisha tunapambana ili tupate matokeo mazuri, tunafahamu timu pinzani wanatupania lakini hiyo haitufanyi tupate hofu na badala yake kila mchezaji anajituma na kutimiza majukumu yake ingawa tunafahamu kuwa upinzani utakuwa mgumu,” alisema Bocco.

 

The post Bocco: Msimu Huu Mgumu kwa Simba appeared first on Global Publishers.



Click to comment
 
Blog Meets Brand