-->

Type something and hit enter

On
 KIKOSI cha Azam FC kimeanza maandalizi ya kujiwinda na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex.


Azam FC jana, Septemba 29 ilianza kupiga matizi hayo ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya tano ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 4 majira ya saa 1:00 usiku.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


 Timu zote mbili zinaingia ndani ya uwanja zikiwa zimetoka kushinda mechi zao za raundi ya nne ambapo Azam FC ilishinda bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons na Kagera Sugar ilishinda bao 1-0 mbele ya KMC.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zinahitaji kuendeleza rekodi zao ambazo wameziweka ndani ya uwanja.


Azam inahitaji kuendelea kulinda rekodi yake ya Septemba kwa kucheza mechi nne ndani ya dakika 360 bila kupoteza huku Kagera Sugar ikiwa na hesabu za kurejesha makali yake baada ya kuanza msimu kwa kusuasua.


Ikiwa imecheza mechi nne ilipoteza mechi mbili sare moja na ushindi mmoja jambo ambalo halikuwapa furaha wachezaji pamoja na benchi la ufundi.


Yusuph Mhilu, mshambuliaji namba moja ndani ya Kagera Sugar amesema kuwa watapambana kurejesha furaha.

Click to comment
 
Blog Meets Brand