-->

Type something and hit enter

On
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

SIKU chache baada ya winga Mghana Bernard Morrison kusaini mkataba na Simba, amesema mashabiki wa timu yake hiyo mpya wasiwe na wasiwasi kwani hatakuwa na usumbufu kama waliouona akiwa Jangwani.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Mghana huyo amesema kuwa kilichomvutia kutua Simba ni ubora wa kikosi walichonacho, wakiwa na viungo Clatous Chama na Luis Miquissone, pia anataka kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao.

“Kabla ya kusaini Simba niliangalia baadhi ya vitu vikiwemo suala la ubora wa kikosi cha sasa cha hapa, kitu ambacho kimenishawishi kujiunga nao kwa ajili ya kufanya nao kazi kwa msimu ujao.

“Lakini pia mimi kama mchezaji nina malengo yangu ya kutaka kucheza kimataifa na Simba wanayo nafasi hiyo, ndiyo maana nikaona kuna umuhimu wa kujiunga nao kwa ajili ya kuonekana zaidi msimu ujao,” aliweka nukta Mghana huyo.

Soma Zaidi>> Ebitoke Amjia Juu Gigy Money

Nyota huyo Mghana wakati akiwa Yanga anakumbukwa kutokana na matukio yake kadhaa ya utata ambapo baada ya kutua Simba amefunguka kuwa atatulia na kuwaahidi mashabiki wa klabu hiyo kutazama kile ambacho atakifanya uwanjani na kuachana na masuala yaliyopita.

“Mashabiki wa Simba kwa sasa wanachotakiwa kufanya ni kuangalia kile ambacho nitaenda kufanya nikiwa kwao na siyo masuala yaliyopita. Watazame kile ambacho nitaenda kukifanya nikiwa uwanjani kwa ajili ya timu yangu,” alimaliza Morrison.

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment
 
Blog Meets Brand