-->

Type something and hit enter

On
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB
Simba: Bado Kombe Moja Tu

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Simba, wamesema kuwa wataivaa Namungo kibabe kuhakikisha waibuka washindi ili kubeba kombe la tatu msimu huu.Simba na Namungo zitakutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, amesema: “Tunahitaji kushinda mchezo huu ili tuweke rekodi ya kutwaa makombe matatu msimu huu, tayari tumeshachukua mawili ambayo ni Ngao ya Jamii na ligi kuu, hivyo bado hili moja.

“Kikosi kipo vizuri, wachezaji wote 22 wanaendelea na mazoezi katika kambi iliyopo hapa Mbeya, tumeweka kambi ya muda mfupi na Julai 31 (leo Alhamisi) tunatarajia kuondoka kuelekea Sumbawanga.

”Wakati Simba wakiwa na mipango hiyo, Namungo kupitia kwa kocha wao mkuu, Hitimana Thierry, amesema: “Tumewahi kufika huku Sumbawanga na tayari tumeanza mazoezi tangu jana (juzi) Jumanne kwa ajili ya kupambana na Simba kwenye fainali hiyo.

“Naamini siku hizi za kufika na kufanya mazoezi uwanjani hapa zitakuwa msaada mkubwa kwetu kwani tutakuwa tayari tumefahamu hali ya uwanja na mambo mengine ya hapa.”

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB
 
Blog Meets Brand