-->

Type something and hit enter

On
KUHUSU MSIMU UJAO....BEKI YANGA AITAJA SIMBA..!!!

BEKI wa timu ya Yanga, Juma Abdul, amewapongeza Simba kwa kufanikiwa kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20.

Akizungumza na gazeti la BINGWA jana, Abdul alisema pamoja na Simba kutwaa taji hilo kwa misimu mitatu mfululizo wajui msimu wa 2020/21, hawataweza kutetea tena.

Abdul alisema watahakikisha msimu unaokuja ubingwa wa ligi hiyo, unatua Jangwani baada ya kuukosa kwa miaka mitatu mfululizo.

Hata hivyo, Abdul alisema walichokifanya Simba si jambo  geni, kwani waliwahi kutwaa ubingwa mara tatu mfululizo kabla yao.

 “Kwa nafasi yangu nawapongeza Simba  kwa kuwa mabingwa wa ligi  na wamefanya jambo ambalo tulilifanya Yanga miaka mitatu iliyopita,”

“Lakini ubingwa huu usiwape kiburi cha kuona wamemaliza na msimu ujao wataweza kuchukua tena, hicho kitu hakitotokea wajue hili kabisa, tutakuja kivingine na lazima ubingwa tuchukue,” alisema
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB