-->

Type something and hit enter

On
Kocha Wa Simba Agomea Mastaa Wake Kupanda Lori

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck amegomea wachezaji wake kupanda gari la wazi lililoandaliwa maalum na uongozi wa klabu hiyo kwa lengo ka kutembeza kombe la ubingwa.

Simba iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere majira ya sa 2:40 asubuhi kisha kuendelea kukaa ndani mpaka pale walipoanza kutoka saa 9:18 asubuhi.
Kocha wa Simba ndiye aliyeanza kutoka nje ya vyumba vya uwanja huo na kuelekea upande yalipokuwa yamepaki magari ya mashabiki na gari maalum ambalo liliandaliwa kuwabeba wachezaji.

Kisha baada ya dakika moja akarudi tena ndani lakini wakati akiwa mlangoni akaonekana kuanza kuzozana na mwanadada Lispa Hatibu ambaye ni msaidizi wa ofisa Mtendaji mkuu wa Simba Senzo Mazingisa.

Mabishano hayo yalidumu kwa dakika moja kabla ya wahudumu wa uwanja na kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola kuwasihi waache ndipo Lispa alipoamua kuondoka kwa hasira huku akifoka.

Inadaiwa chanzo cha mzozo huo ni Sven kugoma wachezaji kupanda gari la wazi ambalo lilipangwa kupita katika barabara mbalimbali za Dar es Salaam mpaka makao makuu ya klabu hiyo Msimbazi huku yeye akitaka timu kwenda moja kwa moja kambini kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumapili.
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB