-->

Type something and hit enter

On
Bushoke Amrudisha K-Lynn Kwenye Game

KAMA ilivyokawaida mpendwa msomaji wa kolamu hii ya Yupo Wapi kukuletea waliowahi kuwa mastaa na kisha kupotea, ambapo leo nimekuletea mwanamuziki wa kizazi kipya Ruta Bushoke ambaye alipata ustaa kufuatia ukali wa ngoma zake kadhaa ikiwemo Barua, Mume Bwege, Dunia Njia pamoja na Nalia kwa Furaha aliyoshirikiana na K-Lynn na Usiende Mbali aliyoshirikiana na Juliana Kanyomozi na nyinginezo.

Baada ya kimya cha muda mrefu, Bushoke ameanzisha bendi yake iitwayo Urithi ambayo inapiga nyimbo zake pamoja na kugonga kopi ya nyimbo zilizowahi kutamba enzi hizo.

Maongezi kati ya Bushoke na paparazi wetu yalikuwa kama ifuatavyo.

Risasi: Bushoke kwanza mashabiki wa burudani wangependa kujua historia yako kiufupi ulivyoanza muziki.

Bushoke: Mimi natoka kwenye familia ya mzee Maximmilin Bushoke ambaye ni mwanamuziki mkongwe, hilo ndilo kuu lililosababisha nianze muziki nikiwa mdogo sana tukiwa tunaishi Dodoma.

Risasi: Enhe ikawaje?

Bushoke: Nikiwa nasoma Shule ya Msingi Makore iliyopo Dodoma, nilijiunga na wanafunzi wenzangu tukaanzisha kundi letu lililoitwa Makore Exagone, hapo ndipo mzuka wa muziki ukaanza kunipanda.

Risasi: Kuna kipindi ulikuwa ukitoa ngoma kali kila baada ya muda fulani, lakini sasa hivi umekuwa kimya kiasi cha kupigwa ‘ovateki’ na wasanii wanaochipukia nyuma yako kama kina Diamond, Harmonize, Mbosso, Aslay na wengineo?

Bushoke: Muziki wa zamani kipindi chetu na sasa hivi ni tofauti, sisi tulikuwa tukiweka nguvu kubwa kwenye muziki lakini wenzetu wanaweka nguvu kubwa kwenye kiki kuliko muziki, unakuta mwanamuziki eti analindwa na mabaunsa kibao mpaka unajiuliza huyo adui akudhuru kwa lipi? Hivyo, hizi kiki zao ndiyo zinawapandisha kwakuwa

Mashabiki wa siku hizi nao wanapenda vitu hivyo.

Risasi: Kwani wewe hupendi kiki?

Bushoke: Mimi sipendi kabisa hizo kiki zao haswa hizo za mabaunsa, napenda kuishi huru katika jamii.

Risasi: Ngoma yako uliyoshirikiana na K-Lynn; Nalia kwa Furaha, ilikuwa gumzo ndani na nje ya Bongo, vipi kwasasa unapowasiliana naye mnajadiliana nini kuhusu muziki?

Bushoke: Tunajadiliana mambo mbalimbali ya kimaisha, lakini suala la yeye kuendelea na muziki tangu aolewe isingekuwa rahisi kwakuwa muziki una mambo mengi, naye mumewe alikuwa mtu mzima, hivyo haikuwa rahisi na hata sasa mumewe amefariki lakini bado kuna masuala ya familia anafuatilia kuyaweka sawa, ila akitulia ntamshauri aje tuendeleze kipaji chetu maana akiachana kabisa na muziki, ni sawa na kuua kipaji chake.

Risasi: Vipi ratiba ya bendi yako Urithi ikoje.

Bushoke: Urithi Band kama kawa kila Alhamisi na Jumamosi tunapiga shoo hapa Dodoma ambapo ndiyo tumepiga kambi kwasasa.

Risasi: Vipi kuhusu familia umeoa?

Bushoke: Bado kidogo sijaoa, ila namshukuru Mungu nina watoto watatu ambapo wakike wawili na wakiume mmoja

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB